Radio D 1 | Kujifunza Kijerumani | Deutsche Welle

Paula na Philip ni wahariri wa Radio D wanaochunguza visa vya ajabu. Andamana na wachunguzi hawa shupavu kote Ujerumani na uimarishe Kijerumani chako na uwezo wa kusikiza na kuelewa pia.

0 Likes     0 Followers     1 Subscribers

Sign up / Log in to like, follow, recommend and subscribe!

Website
http://www.dw.de/dw/0,,10791,00.html?maca=kis-DKpodcast_radiod1_kis-4110-xml-mrss
Description
Paula na Philip ni wahariri wa Radio D wanaochunguza visa vya ajabu. Andamana na wachunguzi hawa shupavu kote Ujerumani na uimarishe Kijerumani chako na uwezo wa kusikiza na kuelewa pia.
Language
πŸ‡°πŸ‡ͺ Swahili
last modified
2019-01-11 16:57
last episode published
2009-08-25 23:20
publication frequency
0.05 days
Contributors
DW.COM | Deutsche Welle author   owner  
Explicit
false
Number of Episodes
26
Rss-Feeds
Detail page
Categories
Education K-12 Higher Education Language Courses

Recommendations


Episodes

Date Thumb Title & Description Contributors
25.08.2009

Tukio 26 – Kumuaga Ayhan

Hali ya huzuni imetanda katika afisi za Radio D. Ayhan anawaaga wenzake na anarudi nchini Uturuki. Ingawa wafanyikazi wenzake wamemwandalia hafla ya kumuaga, hawana la kuchangamkia. Paula anafika kazini asubuhi na kuwapata watu wote wakijitayarisha kw...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 25 – Kuzikaribisha Meli

Waandishi habari hao wanajitahidi kuelewa kauli"getΓΌrkt" na wanazuru bandari isiyo ya kawaida ambako kila meli hukaribishwa kwa namna ya kipekee. Katika Bandari ya Willkomm-HΓΆft kila meli hukaribishwa kwa wimbo wa taifa la nchi inakotoka. Kwenye mchez...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 24 – Meza ya Mhariri

Bundi Eulalia anawasaidia Paula na Philipp kupata mwelekeo. Wanagundua kuwa wafanyikazi wenzao wa gazeti la Hamburg wanahusika kwenye ulaghai huo. Paula, Philipp na Eulalia wanagundua kuwa wafanyikazi wa gazeti la Hamburg walitunga njama yote ya kuwek...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 23 – Pezi la Papa

Paula na Philipp wanategua kitendawili cha mahali pa kwenda kumwangalia papa na kwa mara nyingine tena wanagundua ulaghai uliohusika. Hata hivyo mwanzoni sababu za tukio hilo si dhahiri moja kwa moja. Wakiwa katika harakati za kumtafuta mwanamichezo w...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 22 – Mwanamichezo Aliyetoweka

Philipp na Paula wanafuata dalili za papa na kugundua jambo la kushangaza. Wanaingiwa na hamu zaidi wanapopata bao la kuteleza kwenye mawimbi ya bahari bila mwenyewe na pia makala ya gazeti inayowachanganya. Wanapoepukana na zogo la umati wa watu, waa...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 21 – Papa katika Hamburg

Katika afisi ya Radio D hali ya joto imezidi mno. Paula na Philipp wanafurahi pale wanapopewa kazi ya kwenda pwani ambako papa ameonekana bandarini. Paula, Philipp na Ayhan wanatatizika kwa kiasi kikubwa. Joto limezidi afisini wala hawana kiyoyozi. Pa...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 20 – Uchunguzi wa Wasikilizaji

Paula na Philipp wanawataka wasikilizaji kutoa maoni yao. Mada ya kipindi ni,"Je kusema uongo ni dhambi?" Wasikilizaji wanaweza kutoa maoni yao kuhusu maduara bandia ya mimea na tabia ya wakulima."Je kusema uongo ni dhambi?" Paula na Philipp wanawauliz...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 19 – Kuingilia Jambo kwa Kina

Ingawa maduara ya mimea yalitengezwa na Wakulima, Eulalia bado anaamini kuna madude yanayoanguka kutoka angani. Katika kuchunguza ulaghai huo, Philipp na Paula wanakwenda baa ya mahali ambako wanazungumza na wanakijiji. Paula na Philipp wametengua kit...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 18 – Uchunguzi wa Usiku

Paula na Philipp wanataka kujua mbivu na mbichi kuhusu maumbo ya duara ya mimea na wanakwenda usiku kuchunguza. Lakini wanachokumbana nacho hakihusu viumbe kutoka angani. Mwenye shamba lenye maumbo ya duara yasiyoeleweka anawatoza watalii ada ya Yuro ...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 17 – Maduara ya Mimea

Paula na Philipp wanakwenda kuchunguza wakati maumbo ya duara yanapogunduliwa kwenye shamba la mahindi. Je kuna dude lililoanguka kutoka angani au kuna mtu anawacheza watu shere? Wakati Ayhna anapowasili katika afisi ya Radio D, nao Paula na Philipp w...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 16 – Ikarus

Waandishi wote wawili wanashangazwa na kisa cha tanzia cha Ikarus, shujaa wa visaasili vya Kigiriki. Paula na Philipp wanaeleza kisa chake. Paula na Philipp wanapomwona mvulana mdogo amevaa vazi la Icarus wanaingiwa na fikra: Wanaamua kukizungumzia ki...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 15 – Mavazi ya Karnivali

Paula na Philipp wanatangaza mara nyingine tena kuhusu Karnivali kutokea barabarani. Wanatambua mavazi tofauti na pia wanajifunza lahaja chache za Kijerumani katika harakati za kazi yao. Afisini Paula analipiza kisasi dhidi ya Ayhan- kwa kutumia tarat...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 14 – Wachawi katika Schwarzwald

Hata baada ya kutatizika sana, hatimaye Philipp anafaulu kurudi salama kutoka Schwarzwald na anajitosa kwenye raha ya Karnivali. Paula wala havutiwi na mila hiyo ya Karnivali. Philipp anafurahia sherehe za Karnivali. Paula anaziona sherehe hizo kuwa f...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 13 – Jumatatu ya Karnivali

Si watu wote wanaofurahia Karnivali. Kazi ya Compu inasababisha waandishi habari hao wawili kwenda Schwarzwald ambako Karnivali inachangamkiwa zaidi. Katika baadhi ya maeneo ya Ujerumani watu wanasherehekea Karnivali kwa furaha kubwa. Katika afisi ya ...
DW.COM | Deutsche Welle author
25.08.2009

Tukio 12 – Barua za Wasikilizaji

Endapo kuna jambo usilolijua, ni bora kuuliza. Mwalimu anajibu maswali yaliyoletwa na wasikilizaji wa Radio D kuhusu matukio yaliyopita. Wasikilizaji wanauliza na mwalimu anajibu kila swali kwa kina. Hii ni fursa nzuri kwa wasikilizaji kutafakari taar...
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 11 – Bundi Anayeongea

Je jina Eulalia linatoka wapi? Compu, Ayhan na Josefine wanachunguza maana ya jina hilo na kupata maana tofauti. Mfanyi kazi mwenzao mhispania ndiye anayewasaidia. Bundi Eulalia anataka kujua maana ya jina lake. Wahudumu wa afisi ya Radio D wanashughu...
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 10 – Mahojiano na Mfalme Ludwig

Philipp anakutana na mwigizaji anayeigiza nafasi ya Mfalme Ludwig katika onyesho la muziki na kumtaka afanye mahojiano naye. Ghafla anatambua sauti yake. Wakati huo huo mgeni asiyetarajiwa atembelea afisi ya Radio D. Katika Kasri la Neuschwanstein, Ph...
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 09 – Muziki wa Ludwig

Philipp pia anapata fununu ya kumtambua mgeni. Anaona tangazo gazetini la onyesho la muziki kumhusu Mfalme Ludwig. Akiwa njiani kwenda kwenye ukumbi, anawahoji watalii wanaozuru kutoka maeneo yote ulimwenguni. Huku Paula akiwa afisini mwake Berlin, Ph...
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 08 – Kumtambua Mgeni

Kwenye Kasri la Neuschwanstein, Paula na Philipp wanamhoji mtu anayedai kuwa Mfalme Ludwig. Paula anagundua jambo linalompa fununu ya kumtambua mgeni huyo asiyeeleweka. Waandishi habari hao wawili wanamrai mtu huyo anayedai kuwa Mfalme Ludwig kukubali...
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 07 – Ludwig, Mfalme wa ajabu

Paula na Philipp wanamtambulisha Mfalme Ludwig kwa wasikilizaji kwenye mchezo wao wa redio. Kuteleza thelujini usiku, hafla kubwa na uvumbuzi wa ajabu ni mambo ya mwanzo Ludwig aliyoyafanya katika wakati wake. Waandishi habari hao wawili wanawarejesha...
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 06 – Mfalme Ludwig alifariki vipi?

Katika Kasri la Neuschwanstein, Paula na Philipp wanakutana na mgeni wasiyemwelewa ambaye amevaa joho la Mfalme Ludwig. Wanafanya uchunguzi kuhusu utata unaogubika kifo cha Ludwig. Mwanamume aliyejitanda mabegani mwake joho la Mfalme Ludwig anajaribu ...
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 05 – Mfalme Ludwig bado yu hai!

Paula na Ayhan wanamkaribisha mfanyikazi mwenzao mpya katika Radio D. Tayari wana jukumu muhimu la kutekeleza. Marehemu Mfalme Ludwig wa Bavaria anasemekana angali hai na kundi hilo linataka kuchunguza kadhia hiyo. Philipp anakutana na wafanyikazi wen...
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 04 – Kumsubiri mfanyikazi mwenza mpya

Wafanyikazi wa kitengo cha uhariri cha Radio D wanamsubiri Philipp. Paula na Ayhan, watakaofanya kazi na Philipp, wanajifurahisha. Philipp haonekani na simu hazifanyi kazi. Philipp amechelewa sana kwa sababu ya hali mbaya ya hewa. Anajaribu kumpigia s...
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 03 – Ziara ya Berlin

Philipp anaelekea Berlin. Hali ya hewa inamtatiza sana. Akiwa safarini, Philipp anajuana na watu kadhaa. Philipp anasafiri kwa gari kwenda Munich anakotumai kupanda ndege ya kuelekea Berlin. Safari yake inachukua muda mrefu zaidi kutoka na mvua kubwa....
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 02 – Simu kutoka Radio D

Philipp hajapata amani yoyote wala utulivu. Baada ya kusumbuliwa na wadudu, inambidi kukabiliana na majirani wasioisha kelele. Anapopigiwa simu asiyoitarajia kutoka Berlin, anaondoka haraka. Usumbufu aliopata kutokana na wadudu si lolote si chochote! ...
DW.COM | Deutsche Welle author
24.08.2009

Tukio 01 – Ziara mashambani (Vijijini)

Philipp, ambaye ni kijana, anasafiri kwa gari kwenda mashambani kumtembelea mama yake Hanne. Anatumai kupunga hewa lakini punde anagundua kuwa mashambani pia kuna vitimbi vyake."Mandhari asilia, raha iliyoje!" Philipp anasema punde anapowasili nyumbani...
DW.COM | Deutsche Welle author